visa_vya_kweli

visa_vya_kweli
Author :
Interpreter :
Publisher :
Publish location :
Dar es salaam Tanzania
(0 Kura)

(0 Kura)
visa_vya_kweli
Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Anecdotes. Sisi
tumekiita, Visa vya Kweli. Kitabu hiki kime- andikwa na Sayyid Ali Akbar Sadaaqat.
Kitabu cha Visa vya Kweli kimekusanya simulizi za visa vya kweli vilivyosimuliwa katika Qur’aniTukufu,
hadithi na riwaya na vyanzo vingine sahihi. Kwa kweli, visa hivi hufundisha maadili mema kwa
wanadamu, hivyo, kitabu hiki tunaweza kukiita kuwa ni cha maadili kwa kuwa visa vilivyoelezewa humu
ni vya kimaadili.
Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo kuna mmomonyoko
mkubwa wa maadili. Kitabu hiki kitawafaa sana vijana walioko mashuleni na vyuoni, halikadhalika watu
wa wazima.
Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kwa lugha ya Kiswahili kwa malengo
yaleyale ya kuwahudumia wasomaji wetu wazungumzao Kiswahili ili wapate kuongeza elimu yao ya dini
na ya kijamii kwa ujumla.
Tunawashukuru ndugu zetu, Dr. M. S. Kanju na Mwl. Aziz Njozi kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi
kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha
kuchapishwa kwake.






