Imam Mahdi(as)

Imam Mahdi(as)
Author :
Editor :
Publisher :
Publish number :
Toleo la kwanza
Publication year :
2014
Publish location :
Tanzania Dar es salaam
Number of volumes :
1
(0 Kura)

(0 Kura)
Imam Mahdi(as)
Kitabu ulichonacho mikononi mwako kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kwa jina la “Imam Mahdi (a.s) Kiongozi wa Zama” kilichoandikwa na Sheikh Mulabah Saleh Lulat.Kitabu hiki kwa ujumla huelezea uwepo wa Imam Mahdi (a.s) ambaye ni Imam wa Zama hizi kama ilivyotabiriwa na mtukufu Mtume (s.a.w.w) mwenyewe. Imam Mahdi (a.s) yuko hai lakini macho yetu hayamuoni kwa vile Allah (swt) amemuweka katika Ghaibat kubra a (ghaibu kubwa), kutokana na urefu wa ghaibu hii watu wengi wamefikia hitimisho kwamba Imam huyu hayupo au alikwisha tokea zamani na kuondoka, kwa hiyo hakuna tena cha Imam Mahdi. Haya ni mawazo ya watu wavivu wa kufikiri na waliokata tamaa. Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alipokuwa anatoa bishara hii ya kuja kwa Imam Mahdi (a.s) kutoka katika kizazi chake alisema kuhusu urefu wa ghaibat yake na akanuliwa akisema kwamba “Ghaibat yake itakuwa ndefu sana kiasi kwamba imani ya kuwepo kwake itabaki kwa watu wachache sana - hawajai hata katika kitengele cha mkono.” Kwa hiyo sio ajabu kwa sasa kuona watu walio wengi kutokuwa na imani ya kuwepo kwake - kwani hilo lilikwisha tajwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kabla.Hadithi sahihi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na suala hili utazikuta ndani ya kitabu hiki, zilizosimuliwa na wanachuoni wote wa Kiislamu - Shia na Sunni.